Meneja Wa Diamond Platnumz SALLAM Afunguka kuhusu Ofisi Mpya Ya DIAMOND PLATNUMZ

       

Hapo Jana Msanii Wa Bongo Flava @diamondplatnumz Alitupia Picha Ya Ofisi Yake Mpya Huku Mgeni Wake Wa Kwanza akiwa ni Mamake Mzazi, Msanii Huyo Ambaye Kila Kunapokucha Anazidi Kuwapa Changa Moto Vijana na Wasanii Wenzake Kwa Kuwa Onyesha Kuwa Haijalishi unapotoka cha msingi zaidi ni kufanya kazi kwa bidii. Mmoja wa Mameneja Wake Diamond, SALAAM Alikuwa na Haya ya Kusema Kuhusu Ofisi Mpya Ya Msanii Huyo “Ametoka kwenye maisha ya kulazimisha mlo mmoja uwe mara tatu, amefungua ofisi iliyoajiri vijana 30 asilimia 95 ya Vijana wanategemewa na familia zao, amefungua studio ya kuwapa vijana wenye vipaji vya kuimba wafanyiwe mziki bure…. Kuna mijitu ambayo inaona ushabiki ndio manufaa na kusema anapenda kujishebedua, kuweni na wivu wa maendeleo na nyie mfanye kama yeye ametoka FROM ZERO TO HERO, Nani asiyekuwa na furaha kumfurahisha mzazi wake Leo, Kijana aliyetoka kulala chumba kimoja watu 6, na ameweza kujiajiri mwenyewe na kuwapa ajira Vijana wenzie ili wasaidie familia zao. “THEY DON’T WANT HIM TO HAVE A BETTER OFFICE TO HELP PEOPLE” in *Dj Khalid’s Office* Congrats @diamondplatnumz 🏾🏾🏾