Idadi ya watu wanaosikiliza (stream) nyimbo za R.Kelly yaongezeka baada ya spotify kuzifuta nyimbo zake kwenye playlist zao

Idadi ya watu wanaosikiliza (stream) nyimbo za R.Kelly yaongezeka baada ya spotify kuzifuta nyimbo zake kwenye playlist zao

Image result for R.Kelly 2018


Mapema mwezi huu Spotify walitangaza sera mpya ya kufuta nyimbo kwenye playlist zao, nyimbo ambazo zina malengo ya chuki na miendeno mibaya ya wasanii, R.Kelly alikuwa mmoja wa wahanga wa sera hizo

Kwa mujibu wa ripoti ya Neilsen Music, idadi ya wasikilizaji (stream) wa nyimbo za R.Kelly imeongezeka kwenye mitandao yote ikiwemo spotify wenyewe

Kabla nyimbo zake hazijafutwa kwenye playlist za spotify, Idadi ya wasikilizaji wa nyimbo za R.Kelly kwa wiki ilikuwa 6,584,000 lakini takwimu mpya za tarehe 10 Mei hadi 16 Mei inaonesha idadi imeongezeka hadi mara 6,676,000