Cyrill katoa jina la Raymond kwenye wimbo wake mpya ‘Cheza Kidogo’.



Rapa na bongo fleva staa Cyrill Kamikaze ametoa jina la Raymond wa WCB aka Rayvanny kwenye wimbo wake mpya ‘Cheza Kidogo’ baada ya uongozi wa WCB kuukana collabo hio siku mbili zilizopita.

Cyrill aliachia wimbo wake mpya na kusema kuwa amemshirikisha msanii kutoka lebo ya WCB, Raymond lakini kupitia akaunti yake ya Twitter, meneja wa Diamond, Sallam Sharaff aliweka ujumbe huu kama kuikata kazi hio “Hakuna Collabo na Raymond, alimuomba Ray amuandikie na apewe melody siku nyingi sana! Hiyo nyimbo hatuuitambui.”

Kid Cyrill alitoa malalamiko yake kupitia instagram huku akidai kuwa walifanya kazi hio kabla Raymond hajaingia WCB. Hatua nyingine aliyochukua Cyrill ni kutoa jina la Raymond kwenye rekodi yake. “Ok nadhani issue ilikuwa ni kumtaja Ray kuwa nimemshirikisha na kiukweli ameshiriki kuandika huu wimbo asilimia 70 nzima na hata kuweka sauti zake na deal tukaikamilisha na kazi tumeifanya kabla Ray hajaenda label mpya kama nilivyo sema jana .. Basi jina nimelitoa.