Nuh Mziwanda ameelezea mpango wake wa kufungua studio yake mpya aliyosema itaitwa ‘Last Born Records’.
Akiongea kwenye kipindi cha 5 Select cha EATV, Nuh alisema vifaa vyote vipo tayari na bado tu sehemu ambayo ataiweka studio yake.
“Vifaa vyote vipo tayari na bado tu sehemu ambayo studio zake zitakuwepo, nina studio yangu ambayo ipo na tayari na vifaa vyote vipo, bado vitu vidogo ianze kazi,Studio itakuwa inaitwa ‘Last Born Records’ na kwa kuanza nitaanza kufanya kazi na Ali kiba huyo ndiye ninayeweza kumuongela kwa sasa ambaye tumeshafanya maongezi”.
Nuh Mziwanda kwasasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Jike shupa’ aliomshirikisha Alikiba.