
Diddy
anaongoza kwenye orodha hii ya wasanii watano wa hiphop wenye pesa
zaidi duniani. Pesa hizi hutokana na muziki na kazi au biashara zingine
wanazofanya kujiingizia kipato.
1] Puff daddy mmiliki wa Revolt Tv, Bad Boy Records na mavazi ya Sean
John anaongoza kwa kuwa na thamani ya dola milioni 700. Mwaka jana
alikuwa na milioni 580 na wanasema kazi na biashara zake ndani ya miezi
sita zimeongeza dola milioni 120 nakufikisha 700.
Ukiacha nilivyokutajia hapo juu Pdd pia anasimamia kinywaji kikali cha Ciroc.

2]
Dr Dre Producer na rapper amechukua namba mbili kwa kuwa na thamani ya
dola za Kimarekani milioni 550. Pesa zake zinatokana na studio ya
Aftermath, Earphones na Headphones za Beats by Dre na mikataba kibao ya
matangazo chini yake.

3]
Sean Carter aka Jay Z Amekalia nafasi hii kwa utajiri wake mwenye
thamani ya dola za Kimarekani milioni 520. Zimetoka kwenye muziki, ziara
za muziki, Wasanii na record lebel ya Rock Nation. Pia pesa anazopata
kutoka timu ya kikapu ya Brooklyn Nets, Mavazi ya Rocawear na Live
Nation kila biashara hapo imempa dola milioni 150 million.

4] Birdman ndio C.E.O Wa Cash Money ambayo pia inamiliki Young Money. Anathamani ya ola milioni 160

5]
50 Cent anabiashara nyingi kama Maji, Energy Drinks, Headphones, Bidha
za G Unit, Muziki na anacholipwa kwenye Filamu. Anathamani ya dola
milioni 140.