Familia Inayofanya Kazi Pamoja The Carters Ya Jay Z Na Beyonce, Huu Mchongo Wao Mwingine.


Mo Money  Mo Money  Mo Money  Mo Money Ndio kinachosema sasa mitaani Marekani baada ya taarifa kusamba kuwa Jay Z Na Mke wake Beyonce wana mpango wakufanya ziara ya show 20 sehemu tofauti nchini humo. Mpaka sasa tarehe ya show haijatajwa na info hizi zinasema mwezi wa sita mwaka huu show zitafanyika.
Fahamu Jay Z amemaliza tour yake ya show 52 iliyompa pesa nyingi sana iliyoitwa “Magna Carta” na Beyonce pia kupitia tour yake ya “Mrs Carter Show” .
Fahamu Jay Z Na Beyonce wamefanya kazi nyingi pamoja kama “Bonnie & Clyde” ,“Crazy in Love”,“Drunk In Love” na “Upgrade U” .