Katika maelezo yake amesema kati ya watu ambao aliwatafuta sana ili kupata msaada wakati muziki unaenda vibaya ni B-dozen, hatahivyo anasema hakupata msaada aliuotegemea
B-dozen amejibu hizo tuhuma, amesema “Katika kipindi ulichonitafuta nikusimamie, sikuwa na uwezo wa kufanya hivyo, na ilifika kipindi wewe pia uliacha kunisukuma na unajua kuna majukumu mengi nafanya, ila sasa tuongee kitu cha maana ili kuendelea kusonga mbele. Mimi kama Dozen nakupa ahadi kama leo utasitisha uamzi wako wa kuacha muziki, nakupa ahadi ya kukupa mchango wa mawazo, mbinu na kadri nitakavyojaliwa ili kukusaidia kurudi unapostahili, Lakini siwezi kukuahidi kwamba tutatengeneza hits”
Source : Clouds Fm