
Wiki hii zilisambaa picha za muigizaji mkongwe Jet Li zilimuonesha akiwa amezeeka (miaka 20 zaidi ya umri wake wa sasa) kwasababu ya kusumbuliwa na matatizo ya moyo na ugonjwa wa ‘hyperthyroidism’
Meneja wa Jet Li, Steven Chasman amezungumza na Washington Post, amesema picha zinazosambaa zimetoka vibaya tu, Jet Li anaendelea vizuri na huo ugonjwa amekuwa akipambana nao kwa miaka 10 hadi sasa
Washington Post limeripoti pia kuwa Jet Li anasumbuliwa na maumivu na majeraha ya miguu kutokana na kushoot filamu za ngumi kwa miaka mingi