Nicki Minaj aliitoa hii taarifa kupitia Instagram Live, kuwa album yake ya “Queen” haitatoka tena mwezi wa sita kama alivyotangaza awali bali tarehe 10 mwezi wa nane
“Album nimepanga kuitoa Agosti 10, nataka kwanza kutoa ngoma uangu ya pili ambayo kiukweli nina hamu nayo sana, na ninataka kuanza kuhesabu siku rasmi hadi album itakapotoka” Nicki minaj alifunguka akielezea mipango yake mipya ikiwemo kuwaalika mashabiki wale studio kuisikiliza album kabla haijatoka
Baadaye aliamua kuwapoza mashabiki wake kwa kuahidi kuwalipia ada na madeni ya mikopo, unaandika kwanini akulipie alafu unaweka hashtag, watakaochaguliwa atawatumia ujumbe dm