
Kwa muda sasa imekuwa ikiripotiwa kuwa Drake ameachana Jordan, brand aliyokuwa akifanya nayo kazi awali na sasa amesaini na Adidas
Pusha T mwenyewe anafanya kazi na adidas kitu ambacho kinaipa nguvu diss track yake kwa Drake hasa kuhusu mpango wa Drake kumtumia mtoto wake kutangaza brand yake mpya na Adidas, Kwenye Disstrack Pusha amerap "Adonis is your son/And he deserves more than an Adidas press run, that's real," na kuna mwingine anasema "But we couldn't know about the child until you started selling sweatsuits and sneakers?"
Inadaiwa kuwa “Adidon” ni jina la Brand ya viatu na sweatsuits mpya ya Drake ambayo imetokana na jina la Adonis, jina la mtoto wa Drake na Adidas.
Imeripotiwa kuwa Drake alikuwa amepanga kutangaza kuhusu mtoto wake kwenye hiyo dili na Adidas, Pusha anasema anataka tu kumtumia mtoto wake ili auze Brand yake kwasababu kamtelekeza hizi siku zote