MAMA WA NICK MINAJ AKANUSHA MWANAYE KUCHUMBIWA


Mwanamuziki Nick Minaj.
Siku chache baada ya staa wa muziki wa Pop, Tanya Maraj 'Nick Minaj' kuonyesha mtandaoni kidole chake kikiwa na pete ya uchumba, mama wa nyota huyo ameeleza kuwa binti yake huyo bado hajachumbiwa.
Akizungumza na mtandao wa TMZ, mama huyo alieleza kuwa hata yeye alishtushwa na taarifa hizo lakini alipomuuliza binti yake alimhakikishia kuwa pete hiyo ni urembo.
Nick Minaj akiwa na mama yake.
"Nimejaribu kumuuliza mara kadhaa,ameniambia siyo ya uchumba hivyo namuamini binti yangu kuwa  pete ile ameivaa kama pambo," alisema mama huyo.
Kuzagaa kwa picha hiyo kuliibua hisia kuwa staa huyo ameingia rasmi kwenye uchumba na mpenzi wake, Meek Mill